Ufunuo wa Yohana 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ufunuo wa Yohana 5 (Swahili) Revelation 5 (English)

Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba. Ufunuo wa Yohana 5:1

I saw, in the right hand of him who sat on the throne, a book written inside and outside, sealed shut with seven seals.

Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N'nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake? Ufunuo wa Yohana 5:2

I saw a mighty angel proclaiming with a loud voice, "Who is worthy to open the book, and to break its seals?"

Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. Ufunuo wa Yohana 5:3

No one in heaven above, or on the earth, or under the earth, was able to open the book, or to look in it.

Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. Ufunuo wa Yohana 5:4

And I wept much, because no one was found worthy to open the book, or to look in it.

Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba. Ufunuo wa Yohana 5:5

One of the elders said to me, "Don't weep. Behold, the Lion who is of the tribe of Judah, the Root of David, has overcome; he who opens the book and its seven seals."

Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote. Ufunuo wa Yohana 5:6

I saw in the midst of the throne and of the four living creatures, and in the midst of the elders, a Lamb standing, as though it had been slain, having seven horns, and seven eyes, which are the seven Spirits of God, sent out into all the earth.

Akaja, akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi. Ufunuo wa Yohana 5:7

Then he came, and he took it out of the right hand of him who sat on the throne.

Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu. Ufunuo wa Yohana 5:8

Now when he had taken the book, the four living creatures and the twenty-four elders fell down before the Lamb, each one having a harp, and golden bowls full of incense, which are the prayers of the saints.

Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, Ufunuo wa Yohana 5:9

They sang a new song, saying, "You are worthy to take the book, And to open its seals: For you were killed, And bought us for God with your blood, Out of every tribe, language, people, and nation,

ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi. Ufunuo wa Yohana 5:10

And made them kings and priests to our God, And they reign on earth."

Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu, Ufunuo wa Yohana 5:11

I saw, and I heard something like a voice of many angels around the throne, the living creatures, and the elders; and the number of them was ten thousands of ten thousands, and thousands of thousands;

wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka. Ufunuo wa Yohana 5:12

saying with a loud voice, "Worthy is the Lamb who has been killed to receive the power, wealth, wisdom, strength, honor, glory, and blessing!"

Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele. Ufunuo wa Yohana 5:13

I heard every created thing which is in heaven, on the earth, under the earth, on the sea, and everything in them, saying, "To him who sits on the throne, and to the Lamb be the blessing, the honor, the glory, and the dominion, forever and ever! Amen!{TR omits "Amen!"}"

Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu. Ufunuo wa Yohana 5:14

The four living creatures said, "Amen!" The {TR adds "twenty-four"}elders fell down and worshiped.{TR adds "the one living forever and ever"}